1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Vifo vyatokea katika mapambano baina ya askari na waasi

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hi

Watu wapatao 65 wameuwawa nchini Pakistan katika mapigano baina ya waasi na wanajeshi kwenye jimbo la kaskazini magharibi mwa Waziristan linalopakana na Afghanistan.

Msemaji wa jeshi jenerali Waheed Arshad ameeleza kuwa askari 20 pia wameuwawa kwenye mapigano hayo yaliyotokea baada ya waasi kushambulia msafara wa kijeshi katika eneo hilo ambalo lina wafuasi wengi wa kundi la waasi wa Taliban.