ISLAMABAD:Uchaguzi mkuu Pakistan tarehe 6 Oktoba | Habari za Ulimwengu | DW | 20.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Uchaguzi mkuu Pakistan tarehe 6 Oktoba

Tume ya uchaguzi nchini Pakistan imetangaza tarehe sita mwezi ujayo kuwa ni siku utakaofanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Msemaji wa tume hiyo Muhammad Dilshad amesema kuwa siku ya mwisho ya kujaza fomu kwa wagombea ni tarehe 27 mwezi huu.

Rais Pervez Musharraf ametangaza kuwa atang´atuka katika cheo cha ukuu wa majeshi iwapo atashinda kipindi kingine cha pili cha uongozi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com