ISLAMABAD:Uchaguzi mkuu kufanyika mapema mwaka ujao | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Uchaguzi mkuu kufanyika mapema mwaka ujao

Uchaguzi mkuu wa nchini Pakistan unapangwa kuanyika mapema mwaka ujao.

Waziri mkuu wa Pakistan Shaukhat Aziz amesena kwamba uchaguzi huo utafanyika mapema mwezi Januari mwaka 2008.

Katika kipindi kisichopungua wiki moja rais Pervez Musharraf alijinyakulia wingi wa kura katika uchaguzi wa rais.

Rais Musharraf anasubiri kuidhinishwa rasmi na mahakama kuu.

Uchaguzi huo wa rais ulisusiwa na vyama vya upinzani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com