ISLAMABAD:Musharaff kung´atuka jeshini iwapo atashinda urais | Habari za Ulimwengu | DW | 18.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Musharaff kung´atuka jeshini iwapo atashinda urais

Wakili wa Rais wa Pakistan Pervez Musharaff ameiambia mahakama kuu ya nchi hiyo kuwa kiongozi huyo atang´atuka katika wadhifa wa ukuu wa majeshi iwapo atashinda uchaguzi mkuu wa urais.

Mahakama hiyo inasikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na vyama vya upinzani dhidi ya mpango wa Musharaff kuwania tena kiti hicho.

Wakili huyo amesema kuwa Musharaff yuko tayari kula kiapo akiwa kama raia iwapo ataidhinishwa na bunge pamoja na bunge la majimbo katika kura za pamoja kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Musharaff ambaye ni mshirika mkubwa wa Marekani anamaliza kipindi chake cha uongozi tarehe 15 Novemba mwaka huu.

Kiongozi huyo ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi mnamo mwaka 1999 amekuwa akipoteza umaarufu kutokana na mambo mbalimbali miongoni mwao ni jaribio lake lililoshindwa la kumfukuza kazi jaji mkuu wa nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com