1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:mapigano yanaendelea nchini Pakistan

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H6

Ndege za kijeshi zinaendelea kushambulia maeneo ya kaskazini mwa Pakistan katika jimbo la Waziristan ambalo lina wafuasi wengi wa makundi ya Al qaeda na Taliban.

Mapigano yanaendelea kwa siku ya tatu huku taarifa za kijeshi zikisema kwamba watu 250 wameuwawa wakiwemo wanawake na watoto.

Maelfu ya watu wanakimbia kutoka katika mji wa Mir Ali katika jimbo hilo la Waziristan Kaskazini.

Mapigano hayo yalianza pale wanamgambo wa Taliban walipoushambulia msafara wa kijeshi siku ya jumapili.