ISLAMABAD:Mahakama Kuu yatengua uamuzi wa Rais Musharraf | Habari za Ulimwengu | DW | 20.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Mahakama Kuu yatengua uamuzi wa Rais Musharraf

Mahakama kuu ya Pakistan imemrejesha madarakani Jaji Mkuu wa nchi hiyo Iftikhar Chaundhry.

Majaji wa mahakama hiyo wamesema kuwa hatua ya Rais Pervez Musharraf kumsimamisha kazi Chaundhry mwezi March mwaka huu ni kinyume na sheria.

Chaundhry amekuwa nembo ya upinzani dhidi ya serikali ya Musharraf, na hukumu hiyo inaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa Musharraf ambaye ameiongoza nchi hiyo bila ya kupata upinzani mkali kwa kipindi cha miaka minane iliyopita.

Uamuzi huo unaweza kuathiri mipango ya Rais Musharraf kutaka achaguliwe tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Wakati huo huo mshambuliaji wa kujitoa mhanga amewaua watu wanne akiwemo polisi mmoja, baada ya kujilipua katika kituo cha ukaguzi kwenye jimbo la Waziristan.

Shambulizi hilo limekuja huku serikali ikiwa katika juhudi za kufanya makubaliano mapya ya amani na wanamgambo wa kiislam katika eneo hilo lililoko kwenye mpaka na Afghanistan.

Mapema jana watu zaidi ya 51 waliauawa katika mashambulizi matatu ya kujitoa mhanga mawili kati ya hayo yalitokea kwenye eneo hilo la kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com