ISLAMABAD.Mahakama kuu kuamua juu ya ugombezi wa Musharaf kabla hajatangazwa rasmi kuwa mshindi | Habari za Ulimwengu | DW | 07.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD.Mahakama kuu kuamua juu ya ugombezi wa Musharaf kabla hajatangazwa rasmi kuwa mshindi

Mahakama kuu ya Pakistan leo hii inatazamiwa kutangaza juu ya uhalali wa ugombea war ais Pervez Musharaf.

Matokea ya mwanzo ya uchaguzi war ais hapo jana katika bunge nchini Pakistan unaonyesha rais Pervez Musharaf ameshinda akijizolea kura 252 kati ya kura 257 zilizopigwa kwenye mabaraza yote ya bunge la nchi hiyo.

Hata hivyo mahakama kuu inasubiriwa kuthibitisha iwapo ugombea war ais Musharraf ulikuwa halali kabla ya kutangazwa rasmi kuwa mshindi.

Akizungumzia juu ya ushindi wake rais Musharaf alisema

’’Demokrasia inamaanisha waliowengi sawa,ikiwa kuna upinzani au hakuna demokrasia inamaanisha waliowengi natumai ni hivyo pia nchini mwako.Ikiwa wengi wanapigia kura kitu fulani basi hiyo ndiyo sheria ya wakati huo na hiyo ndiyo demokrasia.Na sasa nafikiri asilimia 54 au 55 ya wabunge wamenipigia kura mimi.’’

Rais Musharraf aliahidi kuachana na cheo cha amiri mkuu wa majeshi ikiwa atashinda uchaguzi huu na kuapishwa rais wa kiraia ikiwa ni zaidi ya miaka minane baada ya kuingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi ambayo hayakusababisha umwagikaji wa damu.

Musharraf alitegemewa kushinda kinyanga’nyiro hiki baada ya wabunge 160 wa upinzani kujiuzulu kupinga ugombea wake kabla ya uchaguzi na chama cha waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto cha Peoples Party kikisusia uchaguzi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com