ISLAMABAD : Zaidi ya watu 220 wauwawa na dhoruba | Habari za Ulimwengu | DW | 24.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Zaidi ya watu 220 wauwawa na dhoruba

Sehemu za kusini mwa Asia zimeathirika vibaya kutokana na dharoba na mafuriko.

Zaidi ya watu 220 wameuwawa katika matukio yaliosababishwa na upepo mkali na mvua kubwa katika mji wa kusini wa Pakistan wenye idadi kubwa ya watu wa Karachi.Maafa mengi yamesababishwa na kurushwa na umeme wakati majengo na nyaza za umeme zilipoanguka.

Takriban maiti 223 zikiwemo za wanawake na watoto zimepokelewa katika kituo cha ustawi wa jamii cha Edhi tokea hapo jana jioni.

Kusini magharibi mwa India watu 45 wameuwawa kutokana na mvua kubwa na vimbunga ambavyo pia vimesababisha wengine maelfu kukosa makaazi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com