ISLAMABAD: waziri mkuu wa zamani huru kurejea nyumbani | Habari za Ulimwengu | DW | 23.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: waziri mkuu wa zamani huru kurejea nyumbani

Mahakama kuu nchini Pakistan imetoa uamuzi kwamba waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif anaweza kurejea nchini humo kutoka uhamishoni.

Hakimu mkuu Iftikhar Mohamed Chaudhry katika uamuzi wake amesema kwamba bwana Sharif na familia yake wana haki ya kurejea na kuishi nchini Pakistan chini ya haki zote za uraia na kwamba kurejea kwao kusitatizwe na vyombo vya dola.

Nawaz Sharif aling’olewa madarakani mnamo mwaka 1999 na jenerali Parvez Musharraf na baadae alihukumiwa kifungo cha maisha kwa tuhuma za utekaji nyara, kukwepa kulipa kodi na makosa ya jinai.

Waziri mkuu huyo wa zamani alikimbilia uhamishoni nchini Saudi Arabia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com