ISLAMABAD: Waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair ahitimisha ziara yake nchini Pakistan na Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair ahitimisha ziara yake nchini Pakistan na Afghanistan

Waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ameondoka mjini Islamabad baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini Pakistan na Afghanistan. Blair aliwasili mjini Islamabad baadae jumamosi iliopita na kufanya mazungumzo na rais Pervez Musharraf na waziri wake mkuu, Shaukat Aziz, kuhusu ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi na waasi wa kitalibani katika eneo la mpaka na Afghanistan. Jana, Blair aliwatembelea wanajeshi wa Uingereza walioko kusini mwa Afghanistan kabla ya kuendelea mjini Kabul kwa mazungumzo na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com