1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Wapinga jaribio la kuua Bhuto.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E3

Mamia ya waandamanaji wamefanya maandamano, wakifunga njia na kuchoma matairi ya magari katika miji kadha nchini Pakistan wakipinga dhidi ya shambulio lililofanywa dhidi ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhuto.

Wakati huo huo polisi wa Pakistan walikuwa wakiwahoji watu watatu leo kuhusiana na shambulio dhidi ya Bibi Bhuto wakati alipokuwa akirejea nyumbani na kusababisha watu 139 kupoteza maisha.

Watu hao wanahusika na gari ambayo mshambuliaji alitupa bomu mjini Karachi siku ya Alhamis usiku, sekunde chache kabla ya mshambuliaji aliyejitoa muhanga kujilipua katika kundi la watu.

Wachunguzi pia wamewahoji wanamgambo saba walioko jela mjini Karachi ili kupata taarifa muhimu kuhusiana na milipuko hiyo, ameongeza afisa wa polisi , ambaye amekuwa akijishughulisha na uchunguzi wa mashambulizi mengine kadha mjini humo.

Bhuto ameahidi kubaki nchini Pakistan kupambana na wapiganaji na kugombea katika uchaguzi mkuu januari mwakani, uchaguzi unaoonekana kuwa muhimu kwa taifa hilo la Kiislamu kurejea katika utawala wa kiraia.

Kuhusu uchaguzi huo waziri mkuu wa nchi hiyo Shaukat Aziz haoni sababu ya kuzuiwa kwa uchaguzi huo.

Sioni hatua hizi za uchaguzi kuwa zitazuiwa. Pamoja na wagombea kuzuiwa. Ni kweli kwamba tutapaswa kutumia busara zaidi, tutapaswa huenda kubadilisha mbinu zetu kidogo.