ISLAMABAD: Wanajeshi wauzingira msikiti wa Lal Majid | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Wanajeshi wauzingira msikiti wa Lal Majid

Milipuko saba mikubwa na milio ya risasi imesikika katika msikiti wa Lal Majid mjini Islamabad mapema leo.

Wanajeshi wa serikali maafisa wa polisi wa Pakistan wamefyatua risasi kuwashinikiza mamia ya wanafunzi walio ndani ya msikiti huo wajisalimishe.

Walioshuhudia wanasema baada ya milipuko hiyo kusikika maafisa wa usalama wametumia vipaza sauti kuwaonya wanafunzi hao wajisalimeshe la sivyo watabeba dhamana kwa hasara itakayotokea.

Polisi wanasema sehemu ya ukuta unaouzungukua msikiti huo imeangushwa na moja ya milipuko hiyo na polisi wamefyatua gesi ya kutoa machozi.

Hapo awali maafisa wa usalama walimkamata kiongozi wa msikiti wa Lal Majid, Abdul Aziz wakati alipokuwa akijaribu kulikimbia eneo hilo. Wanafunzi takriban 1,000 wamejisalimisha baada ya kukubali watalindwa na kupewa rupia 5,000.

Watu 16 waliuwawa wakati mapambano makali yalipozuka kwenye msikiti wa Lal Majid juzi Jumanne kati ya polisi na wanafunzi.

Mamia ya maafisa wa polisi na wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na magari yenye silaha walilifunga aneo la msikiti huo na kutangaza amri ya kutotembea nje katika kitongoji hicho cha Islamabad kufuatia mapambanao ya Jumanne.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com