ISLAMABAD : Wanajeshi 18 wauwawa katika shambulio | Habari za Ulimwengu | DW | 14.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Wanajeshi 18 wauwawa katika shambulio

Takriban wanajeshi 18 wameuwawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha alipolibamiza gari lililosheheni mabomu dhidi ya msafara wao wa kijeshi kaskazini magharibi mwa Pakistan leo hii.

Shambulio hilo limetokea kwenye barabara karibu na kijiji cha Daznaray kilioko kilomita 50 kazkazini mwa mji wa Miran Shah mji mkubwa katika jimbo la Waziristan ya Kaskazini.

Msemaji wa jeshi Meja Generali Waheed Arshad amesema wanajeshi waliouwawa na wale waliojeruhiwa wanapalekwa hospitali.

Kwa mujibu wa maafisa wa kijeshi maelfu ya wanajeshi wa Pakistaan wamekuwa wakiwekwa kwenye mpaka wa eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hicho kujaribu kuwazuwiya wanamgambo wa Kiislamu waliopigwa marafuku kuanzisha vita takatifu vya jihadi dhidi ya serikali kutokana na shambulio lake la umwagaji damu kwa Msikiti Mwekundu mjini Islamabad wiki hii.

Vikosi vimepelekwa katika maeneo matano ya jimbo la Mpaka wa Kaskazini Magharibi linalopakana na Afghanistan ambapo makundi ya wanamgambo yamekuwa yakizidi kupata nguvu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com