ISLAMABAD: Wafuasi wa Sharif wakamatwa Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 05.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Wafuasi wa Sharif wakamatwa Pakistan

Polisi nchini Pakistan imewakamata wafuasi darzeni kadhaa wa aliekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo,Nawaz Sharif.Hatua hiyo imechukuliwa kabla ya kiongozi huyo wa zamani kurejea Pakistan juma lijalo.Sharif amekula kiapo kurejea Pakistan tarehe 10 Septemba na kuzuia kuchaguliwa tena kwa Pervez Musharraf kama rais kwa awamu nyingine. Nawaz Sharif alipinduliwa na Musharraf katika mwaka 1999 bila ya umwagaji wa damu.Kwa upande mwingine,waziri mkuu mwengine wa zamani,Benazir Bhutto alikuwa na majadiliano mjini Dubai pamoja na wajumbe wa Musharraf,juu ya uwezekano wa kugawana madaraka na Rais Musharraf.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com