ISLAMABAD: Waandamanaji wapinga uvamizi wa Msikiti Mwekundu | Habari za Ulimwengu | DW | 13.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Waandamanaji wapinga uvamizi wa Msikiti Mwekundu

Nchini Pakistan,maelfu ya watu wameandamana katika miji mikubwa,kupinga operesheni ya serikali ya kuvamia Msikiti Mwekundu mjini Islamabad.Waandamanaji wamelaani kile walichokiita “kitendo cha kikatili“ kwenye msikiti huo.Zaidi ya watu 100 waliuawa katika operesheni iliyomaliza mgogoro wa siku nane pamoja na wanamgambo waliojificha ndani ya Msikiti Mwekundu.Hapo awali,serikali ilisambaza maelfu ya polisi katika kile pembe ya nchi, kuimarisha usalama,ikihofia mashambulizi ya kulipiza kisasi.Rais wa Pakistan,Pervez Musharraf amekula kiapo kukomesha itikadi kali,kote nchini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com