ISLAMABAD: Vyama vya kisiasa vyalaani kunyongwa kwa Saddam | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Vyama vya kisiasa vyalaani kunyongwa kwa Saddam

Vyama vya kisiasa nchini Pakistan vimepinga vikali kunyongwa kwa Saddam Hussein vikisema kumnyonga wakati wa sikukuu ya Eid al Hajj kutazusha hasira miongoni mwa waislamu.

Jumuiya ya waislamu nchini Pakistan imesema kuuwawa kwa Saddam Hussein siku ya Iddi kumemfanya kuwa shujaa na kifo chake kitasababisha machafuko ya kikabila nchini Irak. Kiongozi wa jumuiya hiyo, Shujaat Hussain amekiri kwamba Saddam alifanya uhalifu mkubwa dhidi ya wairaki lakini hangepaswa kuuwawa siku ya Iddi.

Wakati haya yakiarifiwa kiongozi wa chama cha kikomunisti nchini India, Jyoti Basu ameeleza kutoridhika kwake na matamshi ya serikali ya India kuhusu kunyongwa kwa Saddam Hussein.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com