1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Viongozi kadha wakamatwa.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A2

Nchini Pakistan , kaimu mkuu wa chama cha waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo anayeishi uhamishoni Nawaz Sharrif pamoja na viongozi wengine kadha wamekamatwa.

Hii inafuatia amri ya rais Pervez Musharraf ya hali ya hatari. Akizungumzia hali hiyo waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhuto amesema kuwa ana wasi wasi na uamuzi wa jenerali Musharraf.

Musharraf , ametetea hatua hiyo kuwa amefanya hivyo kutokana na kuongezeka kwa ghasia na pia wabunge ambao walikuwa wakiidhoofisha nchi.

Amedai kuwa kutochukua hatua yoyote kunaweza kuiingiza Pakistan katika hatari.Wakati hatua ya hali ya hatari ikiwekwa, jaji mkuu aliondolewa madarakani na mahakama kuu kuzingirwa na vikosi vya jeshi. Mahakama hiyo ilikuwa iamue iwapo Musharraf alikuwa na haki ya kugombea tena wadhifa wa urais mwezi uliopita wakati akiwa mkuu wa jeshi.