ISLAMABAD: Umwagaji wa damu waendelea Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Umwagaji wa damu waendelea Pakistan

Si chini ya watu 20 wameuawa nchini Pakistan katika shambulizi la kujitolea maisha muhanga. Shambulizi hilo lililenga msafara wa raia wa Kichina na vikosi vya usalama vya Pakistan. Mripuko huo wa bomu umetokea mji wa Hub katika wilaya ya Baluchistan ambayo tangu takriban miaka mitatu iliyopita imekumbwa na machafuko ya waasi wa kikabila wanaogombea mamlaka ya kujitawala wenyewe.Katika shambulizi jingine la kujitolea maisha muhanga na kulenga taasisi ya polisi,hadi watu 8 waliuawa na 29 wengine walijeruhiwa kaskazini-magharibi ya nchi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com