ISLAMABAD : Sharif awasili Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 10.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Sharif awasili Saudi Arabia

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan na kiongozi wa upinzani nchini humo Nawaz Sharif amewasili Saudi Arabia baada ya kurudishwa kutoka Pakistan leo hii ikiwa ni masaa machache tu baada ya kurudia nchini humo kutoka uhamishoni alikokuwa akiishi kwa miaka saba.

Duru zinasema kiongozi huyo wa zamani wa Pakistan alipokewa na maafisa wa serikali ya Saudi Arabia kwenye uwanja wa ndege katika mji wa bandari wa Jeddah.

Mwanasiasa huyo alikamatwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege kwa Islamabad kwa madai ya rushwa akitokea London.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com