ISLAMABAD: Serikali na waasi wakubali kusitisha mapigano
29 Oktoba 2007Matangazo
Vikosi vya serikali ya Pakistan na wanamgambo wanaowaunga mkono Wataliban wamekubali kuweka chini silaha,baada ya mapambano makali ya siku tatu.Msemaji wa serikali amethibitisha habari hiyo na akaongezea kuwa hadi wanamgambo 35 waliuawa katika mapambano ya siku tatu zilizopita.
Serikali ya Pakistan imepeleka wanajeshi 2,500 katika bonde la Swat,baada ya kuuawa kwa wanajeshi wake 16 katika shambulizi la mwanamgambo aliejitolea maisha muhanga.Vikosi na helikopta za kijeshi zilishambulia vituo vya wafuasi wa Maulana Fazlullah alie na itikadi kali za Kiislamu.