ISLAMABAD: Rais Musharraf atoa mwito wa utulivu Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 13.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Rais Musharraf atoa mwito wa utulivu Pakistan

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ametoa mwito watu wawe watulivu baada ya watu thelathini na wanne kuuawa kwenye ghasia mbaya za kisiasa kuwahi kuikumba nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mingi iliyopita.

Rais huyo alikuwa akiuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Islamabad.

Wafuasi wa Rais Musharraf jana walikabiliana vikali na wafuasi wa Jaji Mkuu aliyesimamishwa kazi, Iftikhar Muhammad Chaudhry, katika barabara za mji wa Karachi.

Rais Pervez Musharraf alimtimua Jaji Chaudhry mwezi Machi kwa madai kwamba jaji huyo alitumia madaraka yake vibaya.

Tangu wakati huo kadhia hiyo ya Jaji Chaudhry imekuwa kichocheo cha uasi dhidi ya serikali ya Pervez Musharraf aliyeingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1997 kwa mapinduzi ya kijeshi.

Makundi ya upinzani yamewashutumu wafuasi wa Rais Musharraf kwa ghasia hizo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com