ISLAMABAD: Pakistan yakanusha madai ya kuwahifadhi viongozi wa Al-Qaeda na Taliban | Habari za Ulimwengu | DW | 12.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Pakistan yakanusha madai ya kuwahifadhi viongozi wa Al-Qaeda na Taliban

Pakistan imekanusha madai kwamba inawaficha viongozi wa makundi ya al-Qaeda na Taliban. Hapo awali mkurugenzi wa ujasusi wa Marekani, John Negroponte, alisema viongozi wa al-Qaeda wamepata maficho nchini Pakistan ambako wanajiimarisha.

Aidha Negroponte amesema Pakistan ni kitovu cha uislamu wa siasa kali.

Waziri wa mashauri ya kigeni Pakistan amesema katika taarifa yake kwamba madai hayo si sahihi.

Inashukiwa kiongozi wa Al Qaeda Osama bin Laden anajificha katika maeneo yanayomilikiwa na makabila nchini Afghanistan katika mpaka wake karibu na Afghanistan.

Negroponte alisema pia kuwa wa al Qaeda wanajiimarisha katika maeneo ya Mashariki ya Kati, kaskazini mwa Afrika na barani Ulaya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com