ISLAMABAD: Pakistan yaionya Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 08.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Pakistan yaionya Marekani

Rais Parves Musharaf wa Pakistan ameionya Marekani katika swala la uvamizi wa kijeshi dhidi ya magaidi wa kundi la Al Qaeda ndani ya Pakistan.

Rais Musharaf amemueleza hayo Seneta Richard Durbin wa Marekani waliokutana mjini Karachi kwamba wazo la Marekani la kufanya mashambulio ndani ya Pakistan halitasaidia na kwamba majeshi yake yata tekeleza operesheni za mapambano dhidi ya ugaidi nchini humo.

Musharaf amesema hayo siku moja baada rais Bush wa Marekani kutamka kuwa wanajeshi wake wana uwezo wa kuwasaka na kuwauwa viongozi wa Al Qaeda ndani ya Pakistan lakini hakusema iwapo nchi yake itaishauri kwanza Pakistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com