1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Operesheni dhidi ya msikiti mwekundu yamalizika

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBji

Jeshi la Pakistan limetangaza kwamba operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa kiislamu kwenye msikiti mwekundu mjini Islamabad imemalizika.

Tangazo hilo linafuatia hatua ya wanajeshi kuwatia mbaroni wanamgambo waliokuwa wamesalia kwenye mahandaki yaliyojengwa chini ya msikiti huo wa Lal Majid.

Wanajeshi wameanza kazi ya kuondoa maiti zilizozagaa kwenye uwanja wa msikiti huo na kuondoa mitego iliyowekwa na wanamgambo.

Wizara ya mambo ya ndani imesema watu takriban 59, wakiwemo wanajeshi 9 wa Pakistan, waliuwawa kwenye uvamizi wa msikiti wa Lal Majid, lakini idadi hiyo inahofiwa huenda ikaongezeka.