ISLAMABAD : Mvutano kwenye msikiti wapamba moto | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Mvutano kwenye msikiti wapamba moto

Hali ya mvutano imezidi kuongezeka kwenye msikiti uliozingirwa katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad kufuatia kuuwawa kwa kupigwa risasi kwa kamandoo mwandamizi wa jeshi la Pakistan na wanamgambo wa Kiislam.

Hayo ni maafa ya hivi karibuni kabisa kati ya wafuasi wa Msikiti Mwekundu na wanajeshi wa ulinzi wa Pakistan.Hapo jana Rais Pervez Musharraf amewaonya wale walijiochimbia kwenye msikiti huo kusalimu amri venginevyo watauwawa.Majeshi na magari ya deraya yamekuwa yakiuzingira msikiti huo ambao mamia ya watu wakiwemo wanawake na watoto wamejichimbia ndani tokea Jumanne.

Sheikh mkuu wa msikiti huo Abdul Rashid Ghazi na wafuasi wake wamesema wako tayari kufa mashahidi kuliko kusalimu amri.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com