1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Musharraf atangaza hali ya hatari

Mohamed Dahman3 Novemba 2007

Mtawala wa kijeshi wa Pakistan Rais Pervez Musharraf ametangaza hali ya hatari leo hii wakati nchi hiyo ikikabiliwa na shinikizo la kisiasa na wimbi la la umwagaji wa damu wa itikadi kali za Kiislam.

https://p.dw.com/p/C77I
Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan.
Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan.Picha: picture-alliance/dpa

Wanajeshi na polisi wamezingira mahkama kuu mjini Islamabad ambayo inatarajiwa kutowa hukumu yake hivi karibuni juu ya uhalali wa ushindi wa Musharraf katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 6 Oktoba.

Kufuatia tangazo hilo matangazo ya vituo binafsi vya televisheni yamekatwa pamoja na mawasiliano yote ya simu.

Mshauri wa Musharraf amesema rais huyo atalihutubia taifa wakati wa usiku na kutowa ufafanuzi juu ya sababu za kutangaza hali hiyo ya hatari pamoja na katiba ya muda.