ISLAMABAD: Msafara wa Jaji Mkuu aliyefurushwa waungwa mkono Pakistan. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Msafara wa Jaji Mkuu aliyefurushwa waungwa mkono Pakistan.

Mamia ya watu wanaomuunga mkono jaji mkuu wa Pakistan aliyefutwa kazi, wameungana naye alipoongoza msafara kuelekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara.

Umati wa watu waliokuwa wakipiga kelele za kumshutumu Rais Pervez Musharraf, ulimsindikiza Jaji Iftikhari Chaudhry katika mji wa Abbottabad kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Jaji huyo anatarajiwa kuwahutubia wanachama wa chama cha wanasheria wa mji wa Abbotabad kuhusu haja ya kulinda haki za raia.

Pakistan imekabiliwa na mzozo wa miezi mitatu kwenye idara ya mahakama kutokana na hatua ya Rais Pervez Musharraf kumfuta kazi Jaji Iftikhari Chaudhry kwa madai ya kutumia vibaya madaraka yake.

Mwezi uliopita watu karibu ya arobaini waliuawa wakati wafuasi wa jaji huyo walipokabiliana na watu wanaoiunga mkono serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com