1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Masharti ya kujisalimisha yakataliwa

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlR

Milio ya risasi na miripuko imesikika upya mapema asubuhi ya leo,nje ya Msikiti Mwekundu nchini Pakistan.Hayo yametokea baada ya serikali kukataa masharti ya kujisalimisha yaliyotolewa na Naibu kiongozi wa Msikiti Mwekundu,Abdul Rashid Ghazi alie ndani ya msikiti huo.Serikali imesema, lazima atoke nje pamoja na wafuasi wake wapatao kama 1,000 baada ya ghasia za siku tatu kusababisha vifo vya watu 19.Naibu waziri wa habari wa Pakistan,Tariq Azeem amesema:

“Serikali haitofanya majadiliano zaidi kwani wakati wa kutosha umeshapotezwa kujaribu kuwashawishi kutoka nje.Sasa wajisalimishe bila ya kutoa masharti yo yote.“

Serikali ya Pakistan inamtuhumu Abdul Rashid Ghazi,kuwa anawatumia wanawake na watoto kama ngao ya binadamu.