1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Majeshi kuvamia msikiti.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkU

Serikali ya Pakistan inawatuhumu watu wanaosemekana kuwa ni magaidi kwa kuwashikilia mamia ya wanawake na watoto katika msikiti mmoja mjini Islamabad.

Kwa kujibu tuhuma hizo , msemaji wa msikiti huo amedai kuwa mamia ya watu wameuwawa katika shambulio la kijeshi dhidi ya jengo hilo la msikiti, dai ambalo maafisa wa Pakistan wanakanusha.

Milio ya hapa na pale ya risasi imesikika tena leo Jumatatu asubuhi wakati rais Pervez Musharraf ameitisha kikao maalum ili kujadili tukio hilo la kuuzingira msikiti kwa muda wa wiki moja sasa , ambapo viongozi wa kidini wenye imani kali wanataka kuleta utawala kama wa Taliban nchini Pakistan. Kiasi cha watu 24 wamethibitishwa kuwa wameuwawa katika mapigano hayo, ikiwa ni pamoja na kamanda wa jeshi aliyepigwa risasi wakati vikosi vyake vilipovunja sehemu ya ukuta unaozunguka eneo hilo la msikiti.