1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Maelfu waandamana dhidi ya Musharraf

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNn

Maelfu ya wanaharakati wa upinzani wameandamana nje ya mahkama kuu mjini Islamabad leo hii kudai kukomeshwa kwa utawala wa Rais Pervez Musharraf.

Musharraf anawania kuchaguliwa tena katika uchaguzi licha ya kushuka kwa umashuhuri wake na kuwepo kwa masuala ya kisheria juu ya cheo chake kama mkuu wa majeshi.Upinzani umesema utasusia bunge iwapo Musharraf atawania uchaguzi huo wakati bado akiwa kwenye cheo chake hicho cha kijeshi.

Musharraf ameahidi kwamba atan’gatukwa wadhifa huo wa kijeshi baada tu ya kushinda kipindi kengine madarakani katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe sita mwezi wa Oktoba.