1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISFAHAN : Iran yan’gan’gania mpango wake wa nuklea

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBya

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amesema kwamba shughuli za nuklea za nchi yake zinakaribia kufikia kileleni.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji ulioko katikati ya Iran wa Isfahan Ahmadinejad amesema serikali ya Iran katu haitoachana na harakati zake za nuklea chini ya shinikizo la mataifa ya magharibi.Kauli yake hiyo inakuja kufuatia matamshi yaliotolewa na mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomu Mohamed El Baradei kwamba Iran ina miaka mitatu hadi minne kuweza kuwa na uwezo na kutengeneza silaha za nuklea.

Rais George W. Bush wa Marekani amesema japo jana kwamba atashirikiana na washirika wake wa Ulaya,Urusi na China kuimarisha vikwazo dhidi ya Iran kwa kukaidi kwake madai ya Umoja wa Mataifa ya kusitisha shughuli zake za kurutubisha uranium.

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema anapendelea utatuzi wa kidiplomasia kwa mzozo huo.