1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IS yamlaumu waziri mkuu mpya wa Iraq, yahimiza mashambulio

Zainab Aziz
29 Mei 2020

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS limemlaumu Waziri Mkuu mpya wa Iraqi, na kumwita kuwa ni wakala wa Marekani. Kundi hilo limewahimiza wapiganaji wake kufanya mashambulio zaidi.

https://p.dw.com/p/3czWI
Irak Regierung wird vom Parlament bestätigt
Picha: picture-alliance/AA/Iraqi Parliament

Katika ujumbe huo unaodaiwa kuwa ni sauti ya msemaji mkuu wa IS Abu Hamza al-Qurayshi, iliyochezwa hapo jana Alhamisi, al-Qurayshi aliuliza kwa nini misikiti inafungwa na watu wanazuiliwa kusali katika msikiti mkuu wa Mecca, akiashiria kwamba Waislam hawawezi kudhurika kwa virusi vya Korona.

Mlipuko wa virusi vya corona umevuruga ibada za waisilamu katika Mashariki ya Kati na duniani kote. Nchini Saudi Arabia kuliwekwa karantini mwishoni mwa mwezi Machi ambapo iliwapiga marufuku raia wake na wakaazi wengine kutekeleza Hija ndogo katika mji wa Makka.

Waziri Mkuu mpya wa Iraq Mustafa al-Kadhimi, aliyekuwa zamani mkuu wa idara ya ujasusi ya Iraq anayeungwa mkono na Marekani, aliiingia madarakani mapema mwezi huu baada ya kuwemo kwenye harakati za mapambano dhidi ya IS kwa miaka kadhaa. Kundi hilo linalojiita Dola la Kiislamu lilitangazwa mnamo mwaka 2017 kuwa limesambaratishwa nchini Iraq.

Msemaji wa IS katika ukanda huo amemtaja waziri mkuu mpya wa Iraq kuwa ndiye mwiba wenye sumu kwa kundi hilo la IS na amewahimiza wapiganaji wa kundi hilo kuzidisha mashambulio nchini Syria, Iraq na katika nchi zingine.

Msemaji wa IS katika ukanda huo amemtaja waziri mkuu mpya wa Iraq kuwa ndiye mwiba wenye sumu kwa kundi hilo la IS
Msemaji wa IS katika ukanda huo amemtaja waziri mkuu mpya wa Iraq kuwa ndiye mwiba wenye sumu kwa kundi hilo la ISPicha: picture-alliance/AP Photo/Aamaq News Agency

Katika wiki za hivi karibuni, wapiganaji hao wenye msimamo mkali wa dini ya Kiislamu wamelitumiajanga la corona kama fursa ya kufanya mashambulio katika maeneo ya zamani waliyoyadhibiti katika nchi za Iraq na Syria.

Siku ya Jumatano, wapiganaji wa IS walikishambulia kituo cha serikali ya Syria

Katika eneo la kaskazinina kuwaua askari wanane. Wanajeshi wa Urusi walilipiza mashambulio hayo kwa kuwauwa wapiganaji 11, kulingana na wanaharakati wa upande wa upinzaji.

Ukanda uliochezwa siku ya Alhamisi ulikuwa ni wa tatu kutolewa na msemaji mpya wa IS al-Qurayashi, tangu aliposhika wadhifa huo. Mnamo mwezi Januari, alisema kundi hilo litaanza mashambulio makali kuilenga Israel na aliupuuza mpango wa Marekani wa amani kati ya Israel na Palestina uliodumu kwa miongo kadhaa.

Chanzo: APE