1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ireland kubana matumizi

Kabogo Grace Patricia25 Novemba 2010

Hatua hiyo inalenga kutatua mzozo wa madeni wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/QHc5
Waziri Mkuu wa Ireland, Brian Cowen.Picha: AP

Serikali ya Ireland imetangaza hatua ngumu za kubana matumizi zenye lengo la kusaidia kutatua mzozo wa madeni wa nchi hiyo.

Pamoja na kupunguza matumizi na kuongeza kodi, kutakuwa na upunguzaji wa mshahara wa kima cha chini na ajira kwa maelfu ya wafanyakazi wa umma zitafutwa.

Mpango huo wa miaka minne unalenga kupunguza matumizi kwa kiasi Euro bilioni 15. Serikali hiyo pia inajadiliana kuhusu kupatiwa mkopo wa fedha na Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, unaotarajiwa kuwa na thamani ya karibu Euro bilioni 85.

Waziri Mkuu wa Ireland, Brian Cowen, ambaye serikali yake inakaribia kuvunjika, amedai kuwa mipango yake hiyo itarejesha tena imani iliyotoweka.