Iran yatishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mataifa ya magharibi. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Iran yatishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mataifa ya magharibi.

Tehran.

Iran imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mataifa ya magharibi kuhusiana na vikwazo vya baraza la usalama la umoja wa mataifa vinavyohusu mpango wake wa kinuklia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Manouchehr Mottaki anaripotiwa kuwa ametuma barua kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ambapo anapinga azimio la vikwazo vya hivi karibuni kuwa ni kinyume cha sheria.

Iran inasisitiza kuwa haitatii vikwazo hivyo, ambavyo vilipitishwa March 3, na vina lengo la kuizuwia nchi hiyo kurutubisha madini ya uranium.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com