1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema Marekani "inavuruga" mazungumzo ya nyuklia

Bruce Amani
10 Machi 2022

Iran imeituhumu Marekani kwa kuzifanya kuwa ngumu juhudi za kuufufua muafaka wa nyuklia, baada ya masharti mapya ya Urusi yanayotokana na uvamizi wake wa kijeshi nchini Ukraine kusababisha wasiwasi wa kucheleweshwa zaidi

https://p.dw.com/p/48H48
Österreich | Atomgespräche mit dem Iran
Picha: EU Delegation in Vienna/Handout/AFP

Mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja ambayo yamedumu kwa mwezi mzima mjini Vienna, Austira yalilenga kuirejesha Marekani katika mkataba huo baada ya kujiondoa yenyewe mwaka wa 2018, na Iran kuifanya Iran kupunguza pakubwa shughuli zake za nyuklia.

Soma pia: Iran: Mazungumzo ya nyuklia yamefikia hatua muhimu

Katika siku za karibuni, wanadiplomasia wa Magharibi wameashiria kuwa mazungumzo hayo yamefikia mwisho, na sasa kuiwachia Iran uamuzi wa mwisho.

Ali Shamkhani, katibu wa Baraza Kuu la Kitaifa la Usalama ambalo lina nguvu kubwa, ameandika kwenye mtandao wa Twitter akijaribu badala yake kuilaumu Marekani kwa mkwamo huo.

Iran Atomverhandlungen Ali Bagheri Kani
Mjumbe mkuu wa Iran kwenye mazungumzo ya nyuklia Ali BagheriPicha: Guo Chen/Xinhua/picture alliance

Shamkhani ameandika kuwa mtizamo wa Marekani kwa masharti ya Iran, pamoja na mapendekezo yake yasiyoingia akilini, yanaonyesha kuwa Marekani haina haja ya kuwepo na muafaka thabiti ambao utaziridhisha pande zote. Amesema bila uamuzi wa kisiasa wa Marekani, mazungumzo hayo yataendelea kuwa magumu kila baada ya saa.

Muda mfupi baadaye, ukurasa wa Twitter wa Rais mwenye msimamo mkali Ebrahim Raisi ulionekana kutoa ujumbe wa kiimani kwa uwezekano wa kuunga mkono uwezekano wa kufikiwa makubaliano mjini Vienna.

Aliandika kuwa serikali inafanya mazungumzo katika njia ya mfumo wa kiongozi wa juu Ayatollah Ali Khamenei na haijaachana au haitaachana na masharti yoyote ambayo yalitangazwa. Khamenei ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu masuala yote ya taifa.

Mjumbe mkuu wa Iran Ali Bagheri alijiunga na mazungumzo hayo jana baada ya safari fupi mjini Tehran kwa ajili ya mashauriano.

Mpatanishi mkuu wa Umoja wa UIaya katika mazungumzo hayo Enrique Mora mapema wiki hii alionekana kuashiria kuwa mpira sasa uko mikononi mwa Iran kuamua kama mazungumzo hayo yatafanikiwa au kushindwa.

Alisema hakutakuwa ten ana mazungumzo ya ngazi ya watalaamu wala kufanyika mikutano maalum. Matamshi ya Mora yanaunga mkono yale yaliyotolewa na wajumbe wa Uingereza na Ufaransa. 

Na wakati mazungumzo hayo yakiendelea, jeshi la mapinduzi la Iran lilitangaza Jumanne kuwa imerusha katika anga za mbali satelaiti yake ya uchunguzi.

AP/AFP/Reuters