1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapatiwa pendekezo jipya juu ya mpango wake wa nuklea

Mohamed Dahman3 Mei 2008

Mataifa matano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani yamekubaliana kuipatia Iran mpango mpya wa marupurupu ili kuishawishi kusitisha shughuli zake za kurutubisha madini ya uranium.

https://p.dw.com/p/Dst6
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband.Picha: AP

Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband kwa waandishi wa habari kufuatia mazungumzo mjini London na mawaziri wenzake wa Ujerumani, Urusi China,Ufaransa na Marekani.

Miliband amesema mpango huo wa marupurupu ni sehemu ya mkakati wenye pande mbili katika kushughulikia suala la mpango tata wa nuklea wa Iran.Amesema maelezo kamili juu y mpango huo hayatotangazwa hadharani.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema leo hii wanachotaka mataifa hayo ni kwa Iran kusitisha tu urutubishaji wa uranium katika kipindi hiki cha mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mzozo wa nuklea na nchi hiyo.

Mataifa mengi ya magharibi yanahofu kwamba Iran inaweza kuwa inataka kutengeneza silaha za nuklea hata hivyo Iran yenyewe imekuwa ikisisitiza kwamba mpango huo ni kwa ajili ya dhamira ya amani tu.