Iran yamtimua mwanadiplomasia wa Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Iran yamtimua mwanadiplomasia wa Ujerumani

TEHRAN:

Mwanadiplomasia wa Kijerumani ameamuriwa kuihama Iran katika kile kinachoonekana kama ulipizaji kisasi wa kufukuzwa kwa afisa wa Iran kutoka Ujerumani.

Afisa wa Iran aliamulishwa kundoka katika majira ya kiangazi.

Jarida la habari la Kijeruamni-Der Spiegel-liliripoti mwezi uliopita kuwa Berlin imemfukuza mwanadiplomasia wa Iran kwa madai kuwa alijaribu kununua vifaa fulani kwa ajili ya mpango tatanishi wa Iran wa Nuklia.

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani imehakikisha kuwa mwanadipolamsia wake ameshaondoka Iran, lakini imektaa kutamka chochote kuhusu taarifa za jarida la Der Spiegel au sababu za kuondoka kwa mwanabalozi huyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com