1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaishutumu Marekani kwa "Uraibu wa kupindukia na Iran"

Sekione Kitojo
17 Februari 2019

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad Zarif ameishutumu Marekani kwa kile ilichokiita "uraibu uliopindukia kwa Iran" baada makamu wa rais wa Marekani Mike Pence kusema nchi hiyo inataka kufanya "mauaji ya Holocaust,".

https://p.dw.com/p/3DXUI
Deutschland München MSC Mohammed Dschawad Sarif
Picha: AFP/C. Stache

Hii  "inasikitisha, lakini  wakati  huo  huo ni  hatari  sana," Zarif  alisema   katika mkutano  wa  usalama  mjini  Munich, ambako  alilaani kile  alichokieleza kuwa ni "hotuba za  kijinga za  chuki  zinazotolewa  na  maafisa  wa  Marekani."

Deutschland München MSC Mohammed Dschawad Sarif
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mkutano wa usalama mjini Munich Februari , 2019.Picha: AFP/C. Stache

Pence  alisema  jana  Jumamosi (16.02.2019) kwamba  Iran  inatafuta uwezo  wa kutekeleza "mauaji mengine  ya  Wayahudi ya Holocaust"  na  kutoa wito kwa  washirika  wa  Marekani  katika  bara  la  Ulaya  kufuata kujitoa  kwa Marekani  katika  makubaliano  ya  kinyuklia  na  Iran  ya  mwaka  2015.

Iran  inaishutumu  Iran kwa  kuingilia  katika  mizozo katika  eneo  hilo  na imejitoa  binafsi  kutoka  katika  makubaliano  ya  kinyuklia  na  nchi  hiyo mwaka  jana, na kuiweka  Iran  katika  mzozo  wa  kiuchumi wakati  rais Donald  Trump alipoanzisha  upya  vikwazo  dhidi  ya  taifa  hilo linalosafirisha  mafuta.

Benjamin Gantz, mnadhimu  mkuu  wa  zamani  wa  jeshi  la  Israel, amewataka  wajumbe  waliokuwapo  katika  mkutano  huo  wa  Munich "kutoa amini  maneno  yake  matamu" wakati  wa  hotuba ya  kumjibu  Zarif. "msipumbazwe na  uongo  wake," alisema.

"Kama mnadhimu  mkuu  wa  zamani  wa  jeshi  la  Israel , niliona taarifa  za uhakika  mimi  binafsi kuhusiana  na  kile  kinachotokea nchini  Iran," Gantz alisema. "Kwa  hiyo , naweza  kuwaambia  kwa  uhakika  zaidi  kwamba utawala  ambao  Bwana  Zarif  anauwakilisha ni utawala  wa  uovu."

Munich Security Conference in Munich Mike Pence
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika mkutano wa usalama mjini MunichPicha: Reuters/M. Dalder

Hasimu  mwingine  wa  Iran  hakuwakilishwa  katika  mkutano  huo  baada  ya waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Saudi  Arabia  Adel al-Jubair kufuta uwakilishi  wake  katika  mkutano  huo.

Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani, naibu  waziri  mkuu  wa  Qatar na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni, alitumia  mkutano  huo  kuonya  dhidi  ya hali  inayoongezeka  ya  mgawanyiko  katika  mashariki  ya  kati.

"Tunashuhudia  ongezeko katika  eneo  hili mgawanyiko  na  kwamba  hali hiyo  inaongezeka  siku  hadi  siku,"  amesema.

Juni mwaka  2017 , Saudi Arabia, Umoja  wa  Falme  za  kiarabu, Bahrain  na Misri  zilivunja  uhusiano  wa  kibalozi  na  kibiashara  na  Qatar, zikiishutumu kwa  kuunga  mkono  ugaidi, madai  ambayo  Qatar  inayakana.

55. Münchner Sicherheitskonferenz
Wajumbe wa mkutano wa masuala ya usalama duniani mjini Munich, Februari , 2019Picha: picture alliance/dpa

Wakati  huo  huo Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Iran  amesema  leo kwamba Mataifa  ya  Ulaya  yanapaswa  kufanya  juhudi  zaidi  badala  ya kusema tu iwapo yanataka  kulinda  makubaliano  yenye  lengo  la  kuidhibiti Iran  kutopata  silaha  za  kinyuklia  baada  ya  kujitoa  kwa  Marekani, na kuishutumu  nchi  hiyo  kuwa  ndio "chanzo  kikuu  kwa eneo  la  mashariki  ya kati  kutokuwa  na  uthabiti".

Mohammad Javad Zarif  amesema mjini  Munich  kwamba  mfumo  wa kubadilishana  bidhaa unaofahamika  kama  INSTEX , ambao  umetayarishwa na  Ufaransa, Ujerumani  na  Uingereza  mwezi  uliopita kuruhusu  biashara kuendelea  katika  ya  Iran  na  mataifa  hayo ili  kuepuka  vikwazo  vya  moja kwa  moja  vya  kifedha, na  kuepuka  uwezekano  wa  kuwekewa  vikwazo  na Marekani  hautoshi.

Amesema  kwamba  Ulaya  inapaswa  kuwa  tayari  kulowa iwapo  inataka kuogelea  dhidi  ya  wimbi hatari la  kujitoa  kwa  Marekani  katika makubaliano  ya  kinyuklia.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Zainab Aziz