MigogoroIran
Iran yaionya Marekani dhidi ya uvamizi wa aina yoyote
29 Januari 2026
Matangazo
Ujumbe huo uliandika kwenye mtandao wa X kwamba Iran iko tayari kwa mazungumzo ya kuheshimiana na yenye maslahi kwa pande zote, lakini ikaonya ikiwa italazimishwa, itajilinda na kujibu vikali kuliko ilivyowahi kutokea.
Trump jana Jumatano alirudia tena kutoa vitisho vya kuishambulia Iran akisema muda unakwenda wa kufikia makubaliano ya nyuklia na kusema, kwa kuwa tayari aliitaka Iran kufikia makubaliano, lakini hawakufanya hivyo shambulizi litakalofuata litakuwa la maangamizi kwa taifa hilo.