1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yafurahia ripoti ya upelelezi ya Marekani

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CX6R

Iran imefurahia ripoti mpya iliyotolewa na wapelelezi wa Marekani kuhusu mradi wake wa nyuklia.Ripoti hiyo imeeleza kuwa,Tehran ilisita kutengeneza silaha za nyuklia hapo mwaka 2003. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran,Manouchehr Mottaki amesema,ripoti hiyo imedhihirisha kuwa mradi wa nyuklia wa Iran ni kwa matumizi ya amani.

Kwa upande mwingine,mshauri wa Marekani kuhusu masuala ya usalama,Steven Hadley amesema,ripoti hiyo imeonyesha kuwa sera za serikali ya Rais Bush kuelekea Iran zimefanikiwa.

Hata hivyo,wataalamu waliyotayarisha ripoti hiyo wamesema,Iran imejiachia uwezekano wa kuanzisha upya mradi wake wa silaha za nyuklia.