Iran imekanusha kuishambulia Israel | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Iran imekanusha kuishambulia Israel

Iran imekanusha kuhusika na mashambulizi ya maroketi katika maeneo ya Milima ya Golan inayokaliwa na Israel, ambayo Israel ilisema yalikuwa ya kulipiza kisasi dhidi vituo vya kijeshi vya Iran nchini Syria.

Syrien - Israel | Iran greift Golanhöhen an (picture-alliance/Xinhua News Agency)

Wanajeshi wa Isreal wakiwa katika doria katika eneo la mpakani

Umoja wa Mataifa tayari umetoa wito kusimamisha uhasama, katika wakati huu ambao umegubikwa na hofu ya kuongezeka zaidi kwa hali hiyo.

Mapema leo, Iran imekanusha tuhuma za Israel kwamba imefanya mashambulizi ya maroketi katika maeneo yanayokaliwa na Israel katika milima ya Golan ikieleza ni tuhuma zisizo na msingi zilitolenga kutoa ridhaa kwa Isreal kufanya mashambulizi Syria. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Bahram Qasemi vilevile ameikosoa jumuiya ya kimataifa kwa kutoyalaani mashambulizi ya angani ya Israel ya Alhamisi nchini Syria, ambayo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyaiita ni ya kulipiza kisasi dhidi ya uchokozi wa Iran.

Serikali ya Iran imesema sababu za Israel ni propaganda

Hassan Rouhani (picture-alliance/AP Photo/E. Noroozi)

Rais wa Iran Hassan Rouhani

Waziri huyo alisema ukimya wa taifa lake unaweza kutoa fursa zaidi kwa Israel kuendeleza chokochoko zaidi, ambazo hazina faina yoyote zaidi ya kusabababisha mivutano zaidi katika ukanda huo. Kamati ya ulinzi ya Iran, katika bunge la taifa hilo vilevile imesema haikuwapo sababu yoyote ya kuyashambulia maeneo ya Israel.

Msemaji wa kamati hiyo Mohammed Nabandegani amenukuliwa akisema "Huu ni uongo mwingine, wa Isreal kwa lengo la kufanya propaganda," na kuongeza kwa kukanusha kabisa kwamba Iran haina jeshi lolote nchini Syria.

Awali Alhamis Israel ilitangaza kuwa jeshi lake limeivuruga kabisa miundombinu ya Iran iliyopo katika ardhi ya Syria, katika mashambulizi yake ya angani, walioyaiita ya kulipiza kisasi, baada ya Iran kuvurumisha maroketi 20 katika eneo linalodhibitiwa na Israel la Milima ya Golan. Netanyahu pia alitilia uzito kitendo hicho kwa kusema Iran imevuka mstari mwekundu kwa mashambulizi yake ya maroketi.

Wasiwasi wa biashara ya ndege

Katika hatua nyingine ya hivi punde Iran imesema Iran imeitaka kampuni kutengeneza ndege ya Ulaya ya Airbus kutangaza kama itaendelea na mpango wake wa kuiuzia ndege serikali yake baada ya rais Donald Trump wa Marekani kujiondoa katika makubaliano ya mpango ya nyuklia wa Iran ya mwaka 2015.

Kufuatia hataua hiyo mshauri katika masuala ya uchumi kutoka Uingereza Vicky Pryce anasema: "Kuna masuala mawili. Kwanza kabisa kama Iran imefanya uagizaji wa wowote, watengenezaji wa ndege aina ya Boeng wataathitika. Na pili itakuwaje kama Airbus imekwisha agiza, kwa kuwa baadhi ya vipuri vinatoka Marekani au chochote kutoka Marekani"

Mshauri mwandamizi katika wizara ya barabara, miji na maendeleo wa Iran Asghar Fakhrieh-Kashan aliliambia shirika  la Fars kwamba Airbus itatangaza uamuzi wake katika siku zijazo, hata hivyo Iran bado haitaoa malipo ya awali kwa kampuni ya kutengeneza ndege kwa ajili ya bidhaa zijazo.

Tarehe 8 mwezi huu rais Trump aliiondoa Marekani katika makubaliano ya mwaka 2015 uliohusu mpango wa nyuklia ya Iran, na kuongeza viashiria vya hatari katika mgogoro wa Mashariki ya Kati, kuleta mvurugano kwa washirika wake wa Ulaya na pia kuzusha hali ya kutokuwa sawa katika biashara ya mafuta duniani.

Mwandishi: Sudi Mnette DW Page/RTR/AFP

Mhariri: Gakuba, Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com