1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Intermilan wapepea kileleni mwa Serie A

22 Februari 2021

Intermilan walitoa taarifa kwa mabingwa watetezi Juventus na majirani zao AC Milan baada ya kuwabwaga magoli matatu bila jawabu uwanjani Sansiro hapo Jumapili katika dabi ya Milan.

https://p.dw.com/p/3phrD
Italian Cup | Zlatan Ibrahimovic und Romelu Lukaku
Picha: Antonio Calanni/AP/picture alliance

Lautaro Martinez mshambuliaji kutoka Argentina alicheka na wavu mara mbili kabla Romelu Lukaku hajaugongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la Milan kwa kufunga bao la tatu. Kwa sasa Inter wanaiongoza ligi hiyo wakiwa pointi nne juu ya timu iliyo katika nafasi ya pili.

Inter watakuwa wanakwaana na Genoa Jumapili ijayo huku Milan wanaoishikilia nafasi ya pili wakiwatembelea AS Roma. Juventus wanaoishikilia nafasi ya sita watasafiri kuelekea Verona Jumamosi.