Inter yamsajili Shaqiri kutoka Bayern | Michezo | DW | 09.01.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Inter yamsajili Shaqiri kutoka Bayern

Klabu ya Italia ya Inter Milan imeinyakua saini ya mchezaji wa kasi XHERDAN Shaqiri kutoka mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za vilabu hivyo viwili.

Shaqiri mwenye umri wa miaka 23 ambaye alijiunga na Bayern mwaka wa 2012, amefanyiwa vipimo vya matibabu jana nchini Italia na kusaini mkataba na INTER.

Licha ya kufanya vyema katika mechi kadhaa, Shaqiri alishindwa kujihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha kocha Pep Guardiola na kila mara alidokeza kuhusu uwezekano wa kutaka kuondoka.

Alichaguliwa katika kikosi cha kwanza katika mechi tatu tu kati ya 17 za ligi msimu huu na amefunga jumla ya magoli 11 katika mechi 52 za Bundesliga alizochezea Bayern.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reueters/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com