1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Instanbul na mafuriko

10 Septemba 2009

Watu 32 wamefariki na 9 hawajulikani walipo.

https://p.dw.com/p/JZNm
Abiria wa basi wasubiri kuokolewa.Picha: AP

Mafuriko makubwa yalioukumba mji wa Uturuki wa Istanbul na ule jirani Tekirdag mnamo siku 2 zilizopita yamesababisha vifo vya watu 32 huku wengine 9 wakiwa hawajulikani walipo.Ingawa mvua ilipungua kidogo jana usiku,dharuba mpya na mvua imetabiriwa kesho na keshokutwa Jumamosi.

Watu 26 wamefariki pekee mjini Istanbul,mji mkubwa kabisa nchini Uturuki ukiwa na wakaazi milioni 14-hii ni kwa muujibu wa waziri-mkuu Tayyip Erdogan jana baada ya siku 2 za mvua kali isiowahi kunyesha tangu kupita miaka 80.Watu wengine 5 walifariki Saray,magharibi mwa Istanbul na inaripotiwa wote kutoka ukoo mmoja.Watu wengine 9 hawajulikani walipo.Mjini Istanbul, waokozi baadhi wakiwa ndani ya marekebu wakitumia ngazi kuwasaidia madereva wa magari na malori walionasa katika mafuriko wawasili sehemu za usalama.Ndege za helikopta za kijeshi zikisaidia uokozi.

Mafuriko ya kutisha zaidi yametokea magharibi mwa jiji la Istanbul,sehemu ya ulaya ya Uturuki ambako misingi ya kupitia maji hairidhishi. Mashahidi wamearifu kwamba mawimbi ya matope yakivuta magari,miti na madongo hadi majumbani mwao na majengo mengine mapema jana pale watu walipokaribia kuanza kufuturu baada ya saumu ya mwezi huu wa Ramadhani.

"Tulisikia kishindo kikubwa na halafu tukaona maji yanamiminika yakisukuma magari na madongo." -aliarifu Nuri Bitken, mlinzi wa gereji ya malori.

Tulijaribu kuwaamsha wale madereva waliokuwa bado wamelala katika malori yao,lakini baadhi hawakuwahi kujiokoa.Maiti zao zilibidi ziopolewe kwa mitumbwi. Bitken aliongeza.Kwa bahati nzuri, mji mkongwe wa jiji la Istanbul -maarufu mtaa wa Sultanahmet wenye misikiti maarufu yenye minara mirefu,maqasri ya sultani kandoni mwa bahari na mtaa wa vichochoro wa Beygoglu haikuathrika.

Makamo-mkurugenzi wa Kampuni la bima la AXA SIGORTA, Ali Erlat alisema hasara kutoka mafuriko haya yaweza kufikia kati ya dala milioni 70-80.Waziri wa miundo mbinu Mustafa Demir baada ya kutembelea maeneo ya mafuriko, alisema hasara kubwa imepatikana katika miundo-mbinu ya jiji la Istanbul.

Jiji la Istanbul liko kandoni mwa ujia wa maji wa Bosphorous unaogawa bara la ulaya na Asia na ni mojawapo ya njia muhimu sana za usafiri majini ulimwenguni.

Ingawa mvua zilupungua jana kunyesha,utabiri wa hali ya hewa unasema dharuba na mvua itapiga kesho ijumaa na Jumamosi.Akitembelea jiji hili la Istanbul,waziri mkuu Erdogan aliyaeleza maafa haya "msiba wa karne hii" kwa Uturuki.

Mwandishi: Ramadhan Ali/AFPE

Uhariri: M.Abdul-Rahman