1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

India: Tamasha la ibada kwa waumini wa kihindu lafunguliwa

13 Januari 2025

Umati mkubwa wa mahujaji wa Kihindu nchini India wameoga katika maji wanayoyaita matakatifu leo Jumatatu wakati tamasha la kidini (Kumbh Mela) lilipofunguliwa, watu milioni 400 kushiriki tukio hilo.

https://p.dw.com/p/4p6cm
India | Waumini wakioga katika maji matakatifu
Waumini wa Kihindu wakioga katika maji matakatifu.Picha: R.SATISH BABU/AFP/Getty Images

Kumbh Mela ni tamasha linaloadhimishwa na watu nchini India tangu miaka elfu moja iliyopita ambapo watu hukusanyika kuoga na kufanya ibada zao katika eneo linalounganisha mito mitatu ya Ganges, Yamuna na Saraswati.

Soma pia:Wahindu milioni 400 washiriki katika tamasha kubwa India

Waandaaji wa tamasha hilo wanasema ukubwa wa Kumbh Mela unaweza kujumuisha idadi yote ya watu wa katika nchi za Marekani na Canada.

India ndilo taifa lenye watu wengi zaidi duniani, likiwa na watu bilioni 1.4.