1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India na Ufaransa kuimarisha ushirikiano

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cxva

NEW DELHI: India na Ufaransa zimetangaza mipango ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuanza kushirikiana katika sekta ya nishati ya nyuklia mara tu India itakapoweza kuingia katika soko la kimataifa la nishati ya nyuklia.Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh amesema kuwa amekubaliana na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.Sarkozy alie ziarani nchini India amesema,majadiliano yanayohusika na mitambo ya nishati ya nyuklia yamekamilishwa.