Imran Khan achiliwa huru na maelfu wengine | Habari za Ulimwengu | DW | 22.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Imran Khan achiliwa huru na maelfu wengine

Serikali ya Pakistan imemuachilia huru shujaa wa mchezo wa kriketi aliegeuka kuwa mwanasiasa Imran Khan pamoja na maelfu ya mahabusu wengine waliotiwa mbaroni wakati wakipinga kutangazwa kwa utawala wa hali ya hatari nchini humo.

Khan hapo jana aliingia kwenye mgomo wa kula baada ya kutiwa mbaroni wiki iliopita kwa madai ya ugaidi kwa kujaribu kuongoza maandamano ya wanafunzi dhidi ya Rais Pervez Musharraf.Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif ambaye anaishi uhamishoni nchini Saudi Arabia tokea alipopinduliwa na Musharraf hapo mwaka 1999 amentagaza kwamba yumkini akarudi Pakistan mapema wiki ijayo kushiriki kampeni za uchaguzi iwapo Saudi Arabia itafikia makubaliano na Rais Musharraf ambaye yuko ziarani nchini humo.

Shari f pamoja na Khan wamekuwa wakivitaka vyama vya kisiasa kususia uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwezi wa Januari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com