Imani kali na ugaidi kitisho katika karne ya 21. | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Imani kali na ugaidi kitisho katika karne ya 21.

Mara hii walikuwa ni madaktari, lakini ingekuwa pia wanafunzi, wahandisi ama wauza maduka. Nadharia ya Uislamu wenye imani kali iliyohusika katika jaribio la shambulio lililoshindwa nchini Uingereza haiko tu katika kundi moja la kijamii wataalamu wanasema. Wakati idara za ujasusi duniani kote zikijaribu kufahamu nani atafanya shambulio lijalo, waatalamu kadha wamesema kuwa ugunduzi wa nani hasa anaweza kuwa mpiganaji wa Jihad ni jambo lisilowezekana.

Washambuliaji katika jina la Uislamu wamekuwa kutoka makundi ya vijana hadi watu maarufu wenye taaluma zenye kutukuka, na mtu anayeweza kufanya jaribio jingine anaweza kuwa kijana aliyejifungia katika chumba chake ama jirani yako tajiri nyumba ya pili.

Hakuna uwezekano wa kutoa sura kamili, idara zote za ulinzi ambazo zimejaribu kutoa sura kama hizo kwa kundi la al – Qaeda zimeshindwa, amesema Dominique Thomas, mtaalamu wa mambo ya kijamii kutoka Ufaransa na mwandishi wa kitabu kinachojulikana kama Londonistan. Jihadi katikati ya Ulaya .

Amesema kuwa nadharia hiyo haiwezi kufanyakazi kwa kuwa hivi sasa tunakabiliana na Uislamu wa dunia nzima, na kuongeza kuwa hii ni vigumu kueleweka upande wa mataifa ya magharibi, kwasababu kuna ugumu wa kufahamu kile kinachounganisha Uislamu.

Ulaya na Marekani kuna mtazamo wa Uislamu uliogawanyika baina ya mataifa. Huu ndio mfumo wa ufahamu wetu, lakini sio sahihi. Mafanikio ya manung’uniko ya Uislamu wa kimataifa yamekuja kufuta kila kitu, ameendelea kusema Thomas.

Mtaalamu wa masuala ya akili Marc Sageman , wakala wa zamani wa CIA na mwandishi wa kitabu kipya kinachoitwa jihad isiyokuwa na kiongozi, mfumo wa kigaidi katika karne ya 21, amesisita kuwa , suala muhimu ni kundi hilo na sio tabaka la kijamii.

Mara hii walikutana katika hospitali na mmoja ama wawili kati yao huenda waliwapatia maelezo ya imani kali wenziwao.

Ni kundi ambalo linaimarisha umoja na kuwapa moyo wahusika. Ni nguvu za kundi ndio zinahusika Sageman ameliambia shirika la habari la AFP.

Kundi ambalo lilishindwa katika jaribio lake la kulipua magari mawili yenye mabomu katikati ya London na shambulio lililoshindwa dhidi ya uwanja wa ndege wa Glasgow siku iliyofuata , lina sura kama kundi la mjini Hamburg ambalo lilihusika katika shambulio la Septemba 11 , mwaka 2001 nchini Marekani, ameeleza Sageman.

Wasomi, na watu ambao wanaishi katika jamii ya magharibi , watu hao wanane waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na shambulio hilo nchini Uingereza karibu wote ni madaktari, amesema Sageman.

Lakini , ameendelea kusema tunaweza kutambua kuwa kutokana na mafanikio yao, kumezaa kukata tamaa na masononeko.

Ukiwafananisha na watu wa mitaani , inaonekana kuwa wao wamefanikiwa. Lakini ukiwafananisha na wenzao Waingereza wanafahamu kuwa hawana nafasi katika jamii ya wataalamu wa uganga.

Claude Moniquet, mtaalamu wa ujasusi kuhusiana na mfumo wa mtandao wa Uislamu na mkuu wa kituo cha mikakati ya ujasusi na usalama katika bara la Ulaya kilicho na makao yake makuu mjini Brussels, wakati huo huo amesema jaribio hilo la shambulizi nchini Uingereza linaonyesha kile wataalamu wa masuala ya kijamii wanachokiitwa wawakilishi wa wanao dhalilisha.

Wakati huo huo shambulio la kujitoa muhanga nchini Yemen hivi karibuni , likiwa ni la kwanza la aina yake dhidi ya watalii wa Kimagharibi , linaonyesha kuwa al Qaeda bado ni kitisho katika nchi hiyo masikini licha ya juhudi za kuumaliza mtandao huo.

Haya ni matukio mapya na yanayokera, amesema Nabeel Khoury, naibu mkuu wa ubalozi wa Marekani, akizungumzia shambulio hilo la bomu ambalo limesababisha vifo vya watalii saba kutoka Hispania pamoja na madereva wawili raia wa Yemen katika jengo moja la kale la ibada wiki iliyopita. Khoury amesema kuwa kitisho cha shambulizi kutoka al Qaeda kila wakati kipo licha ya kuwa maafisa wa Yemen wameongeza utaalamu wao

 • Tarehe 08.07.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHBN
 • Tarehe 08.07.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHBN

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com