1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ilhan Omar aapishwa ubunge Marekani

Oumilkheir Hamidou
4 Januari 2019

Ilhan Omar ni mwanamke wa kwanza Muislam mwenye asili ya Afrika kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani.

https://p.dw.com/p/3B2DC
Spika wa bunge Marekani (pili kushoto) akimuapisha Ilhan Omar (pili kulia)
Spika wa bunge Marekani (pili kushoto) akimuapisha Ilhan Omar (pili kulia)Picha: Getty Images/AFP/S. Loeb

Ilhan Omar, mwanamke mwenye umri wa miaka 37, amekuwa Muafrika wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani akiwakilisha jimbo la Minnesota hapo jana.

Mapema, mwanamke huyo aliyeingia Marekani miaka 23 iliyopita akiwa mkimbizi kutoka kambi za wakimbizi nchini Kenya, alituma picha akiwa yeye baba yake kwenye uwanja wa ndege wa Washington DC, akiandika kuwa miongo miwili iliyopita walishuka hapo wakiwa wakimbizi, na sasa wanashuka kuelekea kwenye baraza la Congress.

Ilhan Omar alikuwa pia mwanamke wa kwanza Muislam kuapishwa kushikilia nafasi hiyo hapo jana, akiwa amevaa hijabu. Hii ni baada ya chama cha Democrat, ambacho sasa kinadhibiti Baraza la Wawakilishi, kuamua kubadilisha kanuni ya zaidi ya miaka 100, ambayo ilizuwia watu kuvaa alama za kidini au kuziba vichwa vyao wakiwa ndani ya Baraza hilo.