1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

IDF lashambulia "miundombinu ya kijeshi" ya Hezbollah

30 Novemba 2024

Jeshi la Israel limesema leo kwamba limeshambulia miundombinu ya kijeshi kwenye mpaka wa Lebanon na Syria, ambao hutumiwa na Hezbollah kusafirisha silaha kimagendo.

https://p.dw.com/p/4nbMT
Jeshi la Israel- IDF
Jeshi la Israel, IDF limeshambulia miundombinu ya kijeshi ya Hezbollah likisema wanakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kusafirisha silaha kimagendoPicha: Chameleons Eye/IDF/Newscom/IMAGO

Taarifa ya jeshi imesema ndege zake zilishambulia maeneo hayo yanayotumika kusafirisha silaha kutoka Syria hadi Lebanon.

Katika hatua nyingine, wanamgambo hao wa Hezbollah hii leo wanafanya kumbukumbu ya kiongozi wao aliyeuliwa na Israel, Hassan Nasrallah.

Nasrallah aliuawa Septemba 27, katika makao makuu ya kundi hilo na kumbukumbu hiyo inafanyika kusini mwa Beirut, ambako ni ngome ya Hezbollah.